Teacher Boen Resource Library · Kenya CBC/CBE
Grade 8 · Kiswahili

2.2 Kusoma: Kusoma kwa Mapana – Matini ya Kujichagulia

Mada 2.0 Matumizi yafaayo ya dawa

Kusoma kwa mapana ni kusoma aina mbalimbali za matini (magazeti, vitabu, makala mtandaoni) kwa hiari yako.

Jinsi ya kuchagua matini:

  • Angalia kichwa cha habari – kikivutia.
  • Angalia picha na maelezo mafupi.
  • Soma aya ya kwanza – kama inavutia, endelea.
  • Chagua matini ya kiwango chako (usichague kigumu sana).

Baada ya kusoma:

  • Eleza ujumbe mkuu kwa maneno yako.
  • Andika maneno makuu (msamiati) na maana yake.
  • Tumia kamusi kufafanua maneno.
  • Andika muhtasari mfupi wa kifungu (sentensi 3-5).

Mazoezi:

  • Chagua makala fupi mtandaoni kuhusu matumizi ya dawa. Isome kisha ueleze ujumbe wako.
  • Tafuta maana ya maneno: dawa, tiba, kipimo, daktari, sumu.