Kusoma kwa mapana (extensive reading) ni kusoma vitabu, makala, au nyenzo mbalimbali kwa hiari ya mwanafunzi ili kupanua msamiati na uelewa.
Jinsi ya kuchagua matini bora:
- Angalia kichwa, picha, na maelezo ya jalada.
- Soma aya ya kwanza – ikiwa inavutia, endelea.
- Chagua matini ya kiwango chako (usichague kigumu sana).
- Chagua mada unayoipenda (sports, adventure, fasihi, sayansi).
Baada ya kusoma:
- Eleza ujumbe mkuu kwa wenzako.
- Andika maneno makuu (msamiati) na maana yake.
- Tumia kamusi kufafanua maneno.
- Andika muhtasari mfupi wa kifungu (sentensi 3-5).
Mazoezi:
- Kila mwanafunzi achague makala fupi (mtandaoni au gazeti) kuhusu mazoezi ya viungo (kutembea, kukimbia, kuogelea). Kisha awasilishe ujumbe darasani.
- Tafuta maana ya maneno: mazoezi, viungo, misuli, afya, nguvu.