Shajara (diary) ni maandishi ya kibinafsi yanayorekodi matukio, mawazo, na hisia za kila siku. Shajara si ya kusomwa na watu wengine kwa kawaida.
Vipengele vya shajara:
- Tarehe – kila ingizo lina tarehe.
- Mwanzo – "Nimeamka…", "Leo…", "Jana…".
- Maelezo ya matukio – yaliyotokea kwa mpangilio wa wakati.
- Hisia na mawazo – unahisi vipi?
- Lugha – rahisi, ya kibinafsi, si rasmi.
Mazoezi:
- Andika shajara ya siku tatu ukirekodi mitazamo yako kuhusu usawa wa kijinsia shuleni au nyumbani.
- Badilisha shajara ya mtu mwingine kuwa insha fupi (kwa ruhusa).