Teacher Boen Resource Library · Kenya CBC/CBE
Grade 1 · Kiswahili

8.4 Matumizi ya Hiki na Hivi

Mada ya 8.0 Vyakula vyetu

Tunatumia hiki kuonyesha kitu kimoja cha ngeli ya KI-VI.

Mifano:

Chakula hiki ni kitamu.

Kikombe hiki ni safi.

Tunatumia hivi kuonyesha vitu vingi vya ngeli hiyo.

Mifano:

Vikombe hivi ni safi.

Vyakula hivi ni vizuri.