Ufupisho (summary) ni muhtasari mfupi wa maandishi unaoakisi wazo kuu na hoja muhimu kwa lugha ya mwanafunzi mwenyewe.
Vipengele vya ufupisho mwafaka:
- Soma kifungu kizima kwanza.
- Tambua wazo kuu la kila aya.
- Andika sentensi moja kwa kila aya (sio nakala halisi).
- Usiongeze maoni yako au mifano.
- Dumisha mpangilio wa habari (msimulizi, mjadala, n.k.).
- Ufupisho uwe theluthi moja ya urefu wa asili (takriban).
Mazoezi:
- Soma kifungu kuhusu majukumu ya Bodi ya Barabara ya Kenya au NEMA (National Environment Management Authority). Fupisha kuwa sentensi 5-7.
- Linganisha ufupisho wako na ule wa mwenzako. Angalia kama wazo kuu limebaki.